Pilato wa Al Masr na Simba huyu hapa

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limemteua mwamuzi Boubou Traore kutoka kusimamia mchezo wa kwanza wa Robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kati ya wenyeji Al Masry ya Misri na wawakilishi pekee wa Tanzania, Simba SC.
.
Mchezo wa kwanza kwa Traore kuichezesha Al Masry ulikuwa wa ushindi wa kikosi hicho wa mabao 3-2, ugenini dhidi ya FC Nouadhibou ya Mauritania, katika Kombe la Shirikisho Afrika. .
.
Mechi nyingine ambayo Traore aliichezesha Al Masry, ilikuwa pia ya ushindi wa mabao 2-1, nyumbani dhidi ya RS Berkane ya Morocco, katika Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya kwanza ya robo fainali, mchezo uliofanyika Apr17, 2022.
.
Traore akaendeleza upepo wa bahati kwa miamba hiyo baada ya kuchezesha mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi (kundi D), ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Al Masry ikiwa nyumbani iliitandika Enyimba ya Nigeria mabao 2-0, Novemba 27, 2024.