Mbeya City yaitupa nje Azam FC CRDB Cup

Timu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya usiku huu imeitupa nje Azam FC katika michuano ya kombe la CRDB Cup Kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya 1-1 uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Mbeya City inashiriki Championship hivyo kuitupa nje timu ya Ligi Kuu bara Azam FC inadhihirisha kwamba ushindani Championship ni mkubwa na ndio maana timu hiyo inakamata nafasi ya tatu.

Shukrani zimuendee Riffat Khamis Msuya Kwa kukwamisha penalti ya nne kwa Mbeya City na kuhitimisha safari ya Azam FC msimu huu ikimaliza bila taji lolote.