Kisa cha Aziz Ki kutemwa Burkina Faso ni Hamissa Mobeto

Gazeti moja la kimichezo nchini Burkina Faso limeandika kwamba Stephanie Aziz K ana ugomvi mzito na kocha wa timu ya taifa…

Chanzo cha ugomvi ni huyo ni Hamissa Mobeto.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Aziz K alitoa masharti ya kusafiri na mke wake Mobeto kwenda kuitumikia timu ya taifa.

Yaani mke wake, naye alipiwe gharama zote za safari kuambatana naye hadi Burkina Faso , jambo ambalo limefutiliwa mbali na kocha wa timu ya taifa ya Burkina Faso, Brama Traoré (pichani, kushoto)…

Kocha Traoré katangaza kikosi chake kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 huku Aziz K hajaitwa…

Timu ya taifa ya Burkina Faso “Les Etalons” kwa jina la utani, inajiandaa kumpokea Djibouti Machi 21, na baadae itacheza na Guinea-Bissau Machi 24…

Burkina Faso wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 5, katika kundi A linaloongozwa na Misri wenye alama 10