Jhonier Blanco kutemwa Azam FC

Klabu ya Azam inatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji mwishoni mwa msimu huu ikiwamo kumtema mshambuliaji wa kati, Jhonier Blanco, aliyeshindwa kuonyesha kiwango cha juu tangu alipo jiunga na timu hiyo.

Jhonier Blanco aliyesajiliwa kutoka Rionegro Aguila ya Colombia alitarajiwa kuwa mchezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, lakini hadi sasa ameshindwa kumudu changamoto za Ligi Kuu, akiwa na mabao mawili na pasi moja ya usaidizi wa bao.

Kushindwa kwake kutamba na AzamFC, kumeibua maswali kuhusu uwezo wake wa kuendana na Kasi na ushindani wa soka la Tanzania jambo ambalo limewafanya viongozi wa AzamFC kuanza kujadili uamuzi wa kumwacha mshambuliaji huyo.