Gibrili Sillah awaumiza kichwa Azam FC

Mpaka sasa Gibrill Sillah hajaongeza mkataba mpya na Azam FC, mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu.

Uongozi wa Azam FC bado upo kwenye vikao vya ndani ya bodi kujadili kuhusu ofa ambayo watampatia Gibrill Sillah ili aweze kusaini mkataba ila bado hawajampa ofa Rasmi Sillah.

Gibrill Sillah aliuomba Uongozi wa Azam umuache kwanza autumikie mkataba wake wa sasa na ilifika mwezi wa 4 mwaka huu ndipo atakuwa tayari kukaa na kuzungumzia hatma yake ila kwa sasa anataka kuutumikia mkataba wake kwanza na Focus ni kuisaidia Azam FC.

Ni kweli kuna timu ambazo tayari zimeshaanza kufanya mawasiliano na management ya Sillah kupata Saini yake, Wydad Casablanca na baadhi ya timu kubwa Afrika na Ufaransa.

Kuhusu Yanga, Hakuna taarifa Rasmi, na mpaka sasa Yanga hawajawasiliana na Management ya Sillah wala Sillah Mwenyewe kuhusu Mkataba.