Timu ya Fountain Gate imeendeleza kutoa dozi baada ya kuilaza KMC mabao 2-1 uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam na kuzidi kujikita juu ya msimamo wa Ligi Kuu bara.
Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na kiungo Mrundi mzaliwa wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Elie Mokono dakika ya 77 na 90’+4, wakati la KMC limefungwa na Oscar Paul kwa penalti dakika ya 45.