Benchi lamkimbiza Sidibe Azam FC

Mlinzi wa kushoto Raia wa Senegal Cheick Sidibe amejiunga na klabu ya HJK Helsinki ya Finland akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Azam FC ya Tanzania.

Sidibe ameachana na klabu hiyo baada ya kuwekwa benchi na mzawa Paschal Msindo ambaye amekuwa kwenye kiwango bora kwasasa hadi kuitwa timu ya taifa, Taifa Stars