YANGA SC imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara hasa baada ya kufikisha pointi 72 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote ile, kwa maana hiyo Yanga ni mabingwa msimu wa 2015/16.
Yanga ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Ndanda Fc ya Mtwara uwanja wa Taifa Dar es Salaam, zifuatazo ni picha saba kutoka uwanja wa Taifa Yanga wajisherehekea ubingwa wao waliokabidhiwa na waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba.

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' akinyanyua kikombe cha ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2015/16

Wachezaji wa Yanga wakisherehekea ubingwa wao wa bara

Furaha ikiendelea uwanja wa Taifa wachezaji wa Yanga wakifurahia kikombe cha ubingwa wa ligi kuu bara

Mashabiki wa Yanga wakifyatua mafataki kufurahia ubingwa wa bara

Kocha wa Yanga Mholanzi Hans Van der Pluijm akiwa na baadhi ya wachezaji wa Yanga wakishikilia kombe lao

Kiungo wa Yanga Mzimbabwe Thabani Kamusoko akiwa amemshika mtoto wake akifurahia ubingwa na familia yake wakifurahia ubinhwa

Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga Sc