Yahaya Mbegu arejea Singida Black Stars

Mlinzi wa kushoto Yahaya Mbegu rasmi amerejea klabuni kwake Singida Black Stars na hii ni baada ya muda wake mkopo ndani ya klabu ya Mashujaa FC kutamatika.

Uongozi wa klabu ya Mashujaa umepambana ili kuweza kumbakisha bila mafanikio.

Uongozi wa klabu ya Singida Black Stars umehitaji arejee ili kuanza mapema mipango ya msimu ya ujao.

Mbegu bado amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja na waajiri wake hao kutoka Singida