Twiga Stars kusuka au kunyoa, WAFCON

Timu ya Taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars, inashuka dimbani leo Julai 11, 2025 katika mchezo muhimu dhidi ya Afrika Kusini, ikiwa ni sehemu ya michuano ya WAFCON 2024.

Twiga Stars inashuka dimbani ikitarajia kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo, baada ya kupoteza kwa bao 1-0 katika mchezo wa awali dhidi ya Mali.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 4:00 usiku katika uwanja wa Honner nchini Morocco.

Pia, leo kutakuwa na mchezo mwingine katika mashindano ya WAFCON 2024, ambapo Ghana itakutana na Mali saa 1:00 usiku.