Kibu Denis amaliza majaribio yake Marekani

Kibu Dennis anatarajia kuhitimisha majaribio yake ya wiki tatu ndani ya Nashville SC ya Marekani.

Awali Nashville SC walimpa Kibu wiki mbili za majaribio na Baada ya muda huo kumalizika wamemuongezea wiki nyingine ili wamtazame zaidi.

Nashville SC Ni timu nzuri ambayo inashika nafasi ya pili kwenye Ligi ya MLS Marekani.

Kama Kibu atafaulu majaribio Yake basi klabu hiyo itatuma ofa Simba ili kumununua Mkandaji.

Kibu anapambania ndoto zake Za kucheza Marekani ili awe karibu na familia yake.