Mwanahabari na aliyekuwa Msemaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga, Haji Manara, amechukua Fomu ya kuwania Udiwani katika Kata ya Kariakoo, Jimbo la Ilala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Zoezi la uchukuaji fomu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) linaendelea nchi nzima, ambapo watia nia mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani.