Fadlu ataka Mukwala na Ateba wauzwe


Kocha mkuu wa Klabu ya Simba SC, Fadlu Davies, ameuambia uongozi wa Klabu ya Simba SC Kuwa kama itatokea Ofa Kwa timu yoyote ambayo itahitaji Mshambuliaji Steven Mukwala ama Ateba basi Klabu ifanye biashara hiyo.

Mpaka wakati huu tayari Kuna Vilabu kadha ambavyo vimetuma ofa Kwa Mshambuliaji Ateba bado Kwa Steven Mukwala ambae bado uongozi wa Klabu unatamani kuendelea nae.

Mbadala wa Mshambuliaji mmoja kati ya Hawa wawili itakuwa ni Jonathan Sowah ambae tayari mazungumzo yamekamilika na mda wowote atatangazwa Kuwa Mshambuliaji wa Klabu ya Simba SC.