Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amethibitisha kuwa mlinda lango Aish Manula ni miongoni mwa wa hezaji ambao mikataba yao iko ukingoni_
Hata hivyo amesema hatma ya mlinda lango huyo iko mikononi mwa benchi la ufundi kama watahitaji kuwa nae au la_
"Mkataba wa Manula unamalizika mwishoni mwa msimu lakini wenye jukumu la kuamua nani abaki nani aondoke ni benchi la ufundi"_
"Pamoja na kuwa Manula hakupata nafasi misimu huu lakini hilo halimuondolei sifa yake ya kuwa golikipa bora ambaye timu nyingi zingependa kuwa nawe"_
"Hatma yake itaamuliwa na benchi la ufundi na viongozi kile kitakachoamuliwa tutawajuza wanachama na mashabiki wetu," alisema Ahmed_
Kuna taarifa kuwa Manula yuko mbioni kurejea kwa waajiriwa wake wa zamani Azam Fc, ambapo anasubiri mkataba wake ufikie tamati mwishoni mwa mwezi huu_
Msimu huu umekuwa mgumu kwa Manula kwani hakupata nafasi ya kucheza mechi yoyote ya mashindano_
Shida ilianza baada ya mchezo dhidi ya Yanga msimu uliopita akikaa langoni na kuruhusu mabao matano katika mchezo ambao ulipelekea uongozi wa Simba umsimamishe kuchunguza tuhuma za hujuma.