Mwanamuziki nyota, mchawi wa solo, Omar Seseme wa Sikinde OG amefariki dunia.
Jirani wa Omar Seseme ameiambia Saluti5 kuwa Seseme amefia katika nyumba aliyokuwa akiishi huko Ukonga Majumba Sita.
Jirani huyo aitwae
Kaka Ommy amesema mara ya mwisho Seseme alionekana nje jana usiku.
Hata hivyo Kaka Ommy amesema leo Seseme hakuonekana siku nzima na ndipo ilipofika jioni mlango wa chumba chake ukavunjwa.
"Mlango ulipovunjwa, tukakuta Seseme ameshafariki,'" ameeleza Kaka Ommy.
Kwasasa majirani wanafanya mpango wa kupeleka mwili wa marehemu kuhifadhiwa Amana Hospital, Ilala.