Yanga yalipiza kisasi kwa Tabora United

Yanga SC imefanikiwa kulipa kisasi baada ya jioni ya leo kuifunga Tabora United mabao 3-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Alianza Israel Mwenda dakika ya 21 kwa mpira wa adhabu kabla ya Clement Mzize dakika ya 57 kufunga bao la pili, lakini dakika ya 68 Prince Dube aliifungia Yanga bao la tatu.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 61 ikiendelea kuongoza ligi, wakati washambuliaji Clement Mzize na Prince Dube kila mmoja amefunga mabao 11.

MSIMAMO: NBCPL
1. Yanga Sc—mechi 23—pointi 61
2. Simba Sc—mechi 23—pointi 57
3. Azam Fc—mechi 23— pointi 48
4. Singida BS—mechi 24—pointi 47

MATOKEO MENGINE
FT: Fountain Gate 0-3 Singida Black Stars
FT: Pamba Jiji Fc 1-1 Namungo Fc
FT: KMC Fc 3-2 TZ Prisons