Beki wa upande wa kushoto wa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, Mohamed Hussein Tshabalala au Zimbwe Jr, amesema kwamba kikosi cha sasa cha Simba ni bora kuliko vyote alivyowahi kuitumikia.
Akizungumza hivi karibuni mlinzi huyo wa kushoto mwenye ushawishi mkubwa, amedai mafanikio ambayo msimu huu wameyapata ya kutinga nusu fainali ni moja wapo wa ubora walionao.
"Simba ya sasa ni bora kuliko za misimu yote iliyopita ambayo mimi nimecheza, hii ya sasa acha kusikia ni bora, tunacheza kwa maelewano mazuri nina Imani tutafika fainali au kubeba kombe", alisema Tshabalala.