Namungo, Pamba Jiji hakuna mbabe

Timu ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Pamba Jiji mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza..

Namungo FC walianza kupata bao dakika ya 22 likifungwa na kiungo mkongwe, Jacob Raymond Masawe, kabla ya mshambuliaji Mguinea, Abdoulaye Yonta Camara anayecheza kwa mkopo kutoka Singida Black Stars kuisawazishia Pamba Jiji FC dakika ya 34.