Linah Sanga atamani kuzaa na Darassa

Mwanamuziki wa kizazi kipya Linah Sanga ameweka mambo bayana baada ya kusema anatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za rapper Darassa Cmg.

Muimbaji huyo amesema kwa jinsi ambavyo amewahi kukaa na Darassa na kumsikia akiongea kwa muda mfupi, alibaini kuwa anaweza kuwa baba mzuri sana kwake.

“Ni mtu ambaye ana sifa zote za mwanaume ambaye namtaka. Namchukulia kama kaka yangu yaani sijawahi kumfeel kimapenzi lakini nimekaa naye kwa muda mfupi, nimemuona ni mtu fulani mwenye busara.

Ni mwanaume ambaye nikimuona nasema ‘this guy, I wish ningekuwa nina hisia za kimapenzi naye. Katika wasanii wote I wish my boyfriend angekuwa hivi.”- Linah