TFF yaufungulia CCM Kirumba

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imetangaza kuufungulia Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza kutumika kwa michezo ya ligi baada ya uongozi wa uwanja huo kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
-
Taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa uwanja huo uliofungiwa kutokana na miundombinu yake kutofaa kutumika kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu umefunguliwa baada ya kukaguliwa na kuonekana kukidhi vigezo vya Kikanuni baada ya marekebisho yaliyoelekezwa kufanyika.


-