Simba yaipiga vibaya Dodoma Jiji kama mbwa

Simba SC jioni ya leo katika uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam imetoa kichapo cha mbwa mwizi baada ya kuifunga Dodoma Jiji mabao 6-0 mchezo wa Ligi Kuu bara.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 57 ikicheza mechi 22 sawa na Yanga lakini itaendelea kukaa nafasi ya pili kwani Yanga inaongoza Ligi ikiwa na pointi 58.

Elie Mpanzu alikuwa wa kwanza kuifungia Simba bao dakika ya 16 kabla ya Jean Charles Ahoua dakika ya 20 na 45 kuifungia Simba mabao mawili na kuwa la tatu.

Wekundu hai wa Msimhazi waliongeza bao la nne kupitia Steven Mukwala dakika ya 46, lakini Kibu Denis alifunga mabao mawili dakika ya 54 na 69 na kuhitimisha ushindi wa mabao sita na sasa ligi ikienda mapumziko ya timu za taifa na baadaye Simba ikienda kombe la Shirikisho Afrika