Mkongo wa Tabora United kuiwahi Yanga

Ofisa mtendaji wa klabu ya Tabora United Charles Obiny ameweka wazi kuwa kocha wao Anicet atarejea nchini hivi karibuni kuiwahi mechi yao dhidi ya Yanga. Kwasasa kocha huyo yupo nchini kwao Congo DR akifanya mafunzo ya kuongeza uwezo [Refresher] kwenye ukocha.

“Matumaini yetu hadi kufikia Aprili Mosi atakuwa amejiunga na timu, suala la yeye kufukuzwa kama linavyozungumzwa kwangu halijanifikia ila ninachotambua alituaga anakwenda kufanya kozi yake ya refreshi tu na wala sio vinginevyo,”

- Charles Obiny, Afisa mtendaji mkuu wa Tabora United.