Umri wa Shomari Kapombe wazua utata

Umri wa beki wa upande wa kulia wa Wekundu wa Msimbazi, Shomari Salum Kapombe unazua utata hasa baada ya kuonekana kwa binti wa mchezaji huyo mitandaoni.

Kwa mujibu wa vyeti vya kuzaliwa vya Kapombe vinaonesha kwamba amezaliwa Januari 28, 1992, lakini mtoto wake wa kike aliadhimisha birthday yake hivi karibuni anaonekana kama ana umri wa miaka 20.

Wadau wanashangaa mchezaji huyo kuwa mdogo tena kijana lakini mtoto wake ni mkubwa hivyo wanadai huenda Kapombe anaficha umri wake na ni mkubwa.

Mbali na Kapombe, Meddie Kagere aliyewahi kuichezea Simba miaka kadhaa iliyopita, inasemekana ana mjukuu huko Uganda kutoka kwa binti yake ingawa anasema yeye ni mdogo tena mbichi.