"Mapenzi ni maua" kumtambulisha Zena Omary

Na Ikram Khamees

Mwanamuziki wa kujitegemea wa muziki wa taarabu Zena Omary almaarufu mama Hussein mwenye maskani yake Tandika jijini Dar es Salaam anatarajia kuingia studio kuachia wimbo wake uitwao "Mapenzi ni maua".

Akizungumza na Mambo Uwanjani Blog jioni ya leo, amesema kwamba anaingia studio kuachia wimbo wake mkali ambao anaamini utamweka kwenye ramani.

"Mapenzi ni maua ni wimbo mkali sana ambao naamini utairudisha taarabu kwenye sehemu yake iliyokuwepo hapo nyuma", alisema mama Hussein, kiasili anatoka Kusini mwa Tanzania.

Naye meneja wake Elius January amesisitiza kwamba mama Hussein ni msanii mzuri na wimbo wake unavutia, "jinsi anavyoimba kwa vyovyote muziki wa taarabu unaweza kurejesha mashabiki wake", alidai Elius ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya Efashion.

Mama Hussein aliibuka kwenye taarabu mwaka juzi alipotoa nyimbo zake mbili kwa mkupuo ambazo ni "Ndoa yangu" na "Chuki".

Zena Omary "Mama Hussein" mwimbaji wa taarabu