LADACK CHASAMBI: WINGA MPYA SIMBA ALIYEKUJA NA MOTO

Na Salum Fikiri Jr


HAIKUWA rahisi kwa kiungo mshambuliaji mpya wa Simba SC Ladack Chasambi kusajiliwa na Wekundu hao wa Msimbazi msimu huu.

Kwani timu mbalimbali za ndani na nje ya nchi zilitaka saini yake. 

Nilimsikia mwenyewe mchambuzi nguli Shafih Dauda akimlilia mchezaji huyo, Dauda akutaka Chasambi asajiliwe na Simba, na alikuwa tayari kumtafutia timu nje ya Tanzania. 

Chasambi pia alikuwa anawaniwa na timu nyingine za hapa nyumbani. 

Hatimaye Wekundu wa Msimbazi wakamsainisha mkataba wa miaka mitatu na sasa ni mchezaji wa Simba,.

Licha kwamba usajili wake kuzua gumzo, iliyokuwa klabu yake Mtibwa Sugar ya Turiani, Kilombero mkoani Morogoro kumng' ang' ania ili aendelee kuitumikia timu hiyo, kwani Chasambi ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa wa kuipigania timu yake. 

Tangu asajiliwe na Simba inayonolewa na Muargeria Abdelhak Benchikha bado ajaitumikia vilivyo timu yake, kwani timu hiyo imecheza zaidi ya mechi 6 za Ligi Kuu bara na kombe la Azam Sports Federation Cup, ASFC au kombe la FA.

Mchezaji huyo hakuonekana uwanjani. Simba ilisajili wachezaji sita katika dirisha dogo la Januari mwaka huu ambao ni Saleh Karabaka, Babacar Sarr, Fredie Michael, Pah Omar Jobe, Ladack Chasambi na Edwin Balua. 

Mpaka sasa Jobe, Babacar na Fredie ndio wamecheza mechi kadhaa za Ligi Kuu na kombe la FA na tayari wameshaonyesha viwango vyao, ambapo Wanasimba wameshawaweka kwenye kundi gani. 

Chasambi namba 36

Pia Karabaka naye alionekana kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi na kombe la FA, ambapo uwezo wake umeonekana kama ni kiwango gani, lakini kuanzia Chasambi na balua hawajapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao, ingawa wanafahamika kama ni wachezaji wazuri.

Chasambi ni zao la soka la vijana akilelewa vema na Mtibwa Sugar ambao ni mabingwa mara 4 wa Ligi Kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Chasambi amewakuna Simba kiasi kwamba kuamua kumsajili na hasa kutokana na kiwango chake ndani ya uwanja. 

Mbali ya kuichezea Mtibwa Sugar kwa mafanikio, Chasambi pia aliitwa kwenye timu za taifa ikiwemo Taifa Stars.

Mchezaji huyo aliwahi kujumuhishwa kwenye timu ya taifa iliyomuhisha wachezaji 51 kwa ajili ya kwenda kushiriki michuano ya mataifa Afrika, AFCON zilizomalizika hivi karibuni nchini Ivory Coast. Chasambi aliyezaliwa miaka 19 iliyopita.

Chasambi (Kushoto) akikimbilia mpira

Ni tegemeo la Simba kwa siku za usoni na anatajwa kama mrithi wa Shiza Kichuya aliyewahi kung' ara timu za Mtibwa na Simba pamoja na Taifa Stars.

Chasambi ni winga anayeweza kucheza pande zote za kulia na kushoto, ana ball control, anajua kupiga chenga za maudhi, anajua kutoa pasi zinazofika, anatoa assist na anajua kufunga, tena ana mashuti makali yanayolenga goli. 

Chasambi ni mchezaji chipukizi, bado anajifunza kutoka kwa kaka zake na ndoto zake ni kuipigania Simba na Taifa Stars ili baadaye akacheze soka la kulipwa nje ya Tanzania.

Kikubwa anaweka mkazo kufanya mazoezi kwa bidii na kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja