Mshambuliaji wa Simba, Moses Phiri amejiunga kwa Mkopo katika klabu ya Power Dynamos ya Zambia ambapo atakuwa huko hadi mwisho wa msimu.
Kabla yakupatwa na majeraha yaliomuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu Phiri alikuwa chaguo la kwanza ndani ya kikosi. Uongozi wa Simba unaamini Phiri atakaporejea kikosini atakuwa imara zaidi na kurudi katika makali yake.