ABDALLAH HAMISI RIZIKI: NYOTA MPYA SIMBA, KACHEZA KENYA NA NAMIBIA

Na Salum Fikiri Jr

 ABDALLAH Hamisi ni jina geni lililotajwa katika utambulisho wa klabu ya Simba SC kwenye usajili wa kikosi chake msimu ujao, Abdallah ni mzawa hivyo aliwaacha hoi wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo. 

Wakati anatangazwa wengi walidhani ni mchezaji wa kigeni kama walivyozoea mashabiki wa timu hiyo ambapo wanapenda kusikia mchezaji wa kigeni akitangazwa , lakini Abdallah hatoki nje ya nchi ingawa ametoka Botswana 


Ikumbukwe Abdallah aliwahi kuichezea timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga ambayo ilikuwa inashiriki Ligi Kuu Tanzania bara, akiwa Stand United.

Abdallah alicheza vizuri na akazivutia timu mbalimbali za ndani na nje ya nchi, Muholoni ni moja kati ya timu alizotumikia kabla kutua Bandari iliyoamua kumchukua. 

Abdallah anayecheza nafasi ya kiungo hasa namba sita au nane na pia ana uwezo wa kucheza kama play maker yaani namba kumi, akiwa Tusker Abdallah alifanya vizuri na kuonekana kati ya wachezaji muhimu. 

Kwa hapa nyumbani Tanzania, bado utaratibu wa kuwathamini wachezaji wetu nje ya mipaka yetu sio mzuri sana, kwani Abdallah hakupewa nafasi kwenye timu ya taifa, Taifa Stars ingawa alicheza vizuri. 

Tusker zamani ilifahamika kama Kenya  Breweries ambayo ilitamba sana kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika mashariki na kati ilizidiwa ujanja na wazalishaji sukari wa Sony Sugar ambao waliamua kumchukua kutoka Tusker. 

Abdallah alisifika sana kwa kukaba, anajua kupiga pasi ndefu na ana uwezo mkubwa wa kukaa na mpira na kutoa pasi, Abdallah ana ball control na si muoga kwani ana nguvu na ana akili nyingi za kumtoka adui. 

Kiungo huyo ana mashuti makali na anaweza kufunga, mchezaji huyo anajiamini awapo na mpira na ni ngumu kumnyang' anya mpira mguuni kwake, lakini yeye anaweza kupora mpira miguuni kwa adui yake kwani ni mjanja sana.

Abdallah ni kama kiraka hivyo lile pengo la Erasto Nyoni aliyekuwa na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani, hilo litamalizwa na Abdallah.  

Utapa United waliamua kufanya kweli kwa kumchukua, alifanya vizuri, Simba nao wameamua kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili ambao utamfanya akae hadi msimu wa 2026. 

Abdallah ataisaidia sana Simba kama atapewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, ingawa haitakuwa rahisi Abdallah kuaminika na kuanza kikosi cha kwanza.

Lakini anaweza kuwashangaza kama walivyoweza akina Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein "Zimbwe Jr", Shomari Kapombe, John Bocco na 
Aishi Manula. 



Mchezaji huyo ana malengo yake ya kufika mbali zaidi, kwani kucheza kwake Simba ni moja ya malengo aliyokuwa nayo tangu akiwa mdogo, anaamini Simba itamtoa hadi kucheza soka barani Ulaya ambapo ndoto zake amezielekeza huko. 

Mchezaji huyo aliyezaliwa Novemba 18, .1998 anaamini timu ya taifa, Taifa Stars itatimiza ndoto zake kwani aliwaza sana kuitwa timu ya taifa ni mafanikio makubwa kwake. 

Mbali ya kuzichezea Muhoroni Bandari, Tusker na Sony Sugar, Abdallah pia aliwahi kuzichezea Tarime United na Tarime Worries