Mlinzi wa pembeni Djuma Shabani aliyekuwa anakipiga kwenye kikosi cha Yanga sc misimu kadhaa nyuma huenda akajiunga na Azam fc kabla dirisha halijafungwa.
Taarifa zinaeleza kuwa yupo katika mazungumzo na Azam fc kuona namna ya kukamilisha dili hilo, endapo dili hilo litakamilika Azam fc watalazimika kuachana na mchezaji mmoja wa kimataifa ili kumpisha Djuma Shabani raia wa Drc Congo.