Sikia hii: Sunday Manara ni Mtanzania wa kwanza kucheza soka barani Ulaya

Na Ikram Khamees

Sunday Ramadhan Manara alizaliwa Novemba 23 Mwaka 1952 Barabara ya Kawawa Ujiji Mkoani Kigoma , Ni Mtoto wa Mzee Rama , aliyekuwa Mfanyakazi wa Kampuni ya AMI TANZANIA LTD Bandarini Kigoma ,Kabila lake ni Mmanyema.

Sunday Manara ndio Mtanzania wa kwanza kucheza soka la kulipwa Barani Ulaya na ni Mtanzania wa kwanza kucheza ligi moja na Nguli wa Soka Duniani Edison Arantes Nascimento maarufu kwa jina la #PELE.

Sunday Manara aliichezea klabu ya SC Heracles ya nchini Uholanzi kuanzia disemba 1977 hadi Julai 1978 alipohamia SV St.veit ya Austria,New York eagle ya Marekani na Al-Nasr ya Dubai baada ya awali kuichezea Yanga na Pan Africans za Dar es salaam.