Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Baada ya Yanga Sc jana kuishusha kileleni Simba na kukamata usukani wa ligi, Simba SC jioni ya leo inaumana na Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ugumu kwenye mchezo huo ni kwamba timu zote zinalingana kwa pointi 11, na mechi tano hivyo kila moja ikishinda inakwea kileleni katika msimamo wa ligi, kwa vyovyote mechi itakuwa ya kukata na shoka kwani Simba na Mtibwa zinapokutana shughuri huwa pevu.
Kwa mujibu wa nahodha wa Simba, Method Mwanjale, amesema wachezaji wa Simba wako tayari kwa mchezo wa leo na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuipa sapoti timu yao iondoke na pointi tatu, Yanga inaongoza ligi hiyo baada ya jana kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1