Kiungo wa zamani wa Yanga, Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Athuman Abdallah China ambaye alipata kutamba katika miaka ya 90 na kustaafu soka la ushindani kumbe bado wamo.
China ambaye kwa sasa anaishi nchini Uingereza akifanya kazi katika Uwanja wa ndege wa kimataifa jijini London amekuwa akifanya mazoezi mepesi mepesi ya kuweka mwili wake safi ili kujenga afya.
Nyota huyo aliyesajiliwa na Yanga mwishoni mwa miaka ya 80 akitokea timu ya Printipak na baadaye alienda Uingereza kujaribu bahati ya kucheza soka la kulipwa na aliichezea timu ya Warsal ambayo ilikuwa inashiriki Ligi Daraja la nne