Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
MWANAMUZIKI na kiongozi wa zamani wa kundi la Stone Musica "Wajelajela gwaa" Ndanda Kosovo "Kichaa" raia wa Kongo amefariki dunia leo katika hospitali ya Muhimbili alikolazwa.
Kwa mujibu wa mwanamuziki mwenzake mwenye uraia wa Kongo King Dodoo la Baucha, amesema kuwa Kosovo ambaye awali alilazwa Hospitali ya Mwananyamala amepatwa baada ya kusumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Kosovo aliwahi kutamba na bendi za FM Musica (sasa FM Akademia) na Stone Musica a k a Wajelajela gwaa, Mambo Uwanjani bado itaendelea kuwaletea yanayojiri toka kwenye msiba wa nguli huyo.
MUNGU AILAZE MAHARA PEMA PEPONI