KIPA
Mark Schwarzer amesani Mkataba wa mwaka mmoja Chelsea, baada ya
kuondoka Fulham mwishoni mwa msimu kufuatia kumaliza Mkataba wake.
Kipa
huyo mwenye umri wa miaka 40 amechezea klabu za Bradford City,
Middlesbrough na hivi karibuni Fulham, kwa kipindi cha miaka 17.
"Ni
klabu babu kubwa,"alisema kuiambia tovuti ya Chelsea. "Ni moja ya klabu
kubwa na bora duniani, na ni heshima kusaini Chelsea. Sikushawishiwa
kwa kiasi kikubwa kuja hapa,"alisema.
![Done deal: Schwarzer signing his contract with club Secretary/Director David Barnard](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/07/09/article-2359005-1ABC6389000005DC-289_634x407.jpg)
Dili limekamilika: Schwarzer akisaini Mkataba wake na Katibu na Mkuruenzi wa klabu, David Barnard
Kipa
huyo wa kimataifa wa Australia, ameisaidia nchi yake kufuzu Fainali za
Kombe la Dunia Brazil mwakani, na pia atakuwa nyumba ya kipa namba moja
Chelsea, Petr Cech, ingawa atapata nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika
mashindano mbalimbali.
Ameidakia
mechi 108 Australia, na mafanikio yake makubwa England ni pamoja na
kutwaa Kombe la Ligi akiwa na Middlesbrough mwaka 2003 na kucheza
Fainali za KOmbe la UEFA mwaka 2006 na Europa League mwaka 2010.
![Sharing a joke: Schwarzer meets England duo Frank Lampard and John Terry](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/07/09/article-2359005-1ABC6340000005DC-798_634x392.jpg)
Utani kidogo: Schwarzer amekutana na nyota wa England, Frank Lampard na John Terry
![Meeting the boss: Jose Mourinho was happy to see his new acquisition](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/07/09/article-2359005-1ABC6350000005DC-469_634x434.jpg)
Akiwa na bosi: Jose Mourinho alikuwa mwenye furaha kumuona kipa mpya
![Keeping buddies: Schwarzer and his new teammate Petr Cech](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/07/09/article-2359005-1ABC6384000005DC-727_634x349.jpg)
Makipa wamekutana: Schwarzer na kipa mwenzake mpya, Petr Cech
![Doing the rounds: Belgian striker Romelu Lukaku meets Schwarzer at their Cobham Training Ground](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/07/09/article-2359005-1ABC634C000005DC-290_634x455.jpg)
Na
huyu rasta: Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Romelu Lukaku akiwa
na Schwarzer katika viwanja vyao vya mazoezi huko Cobham