Vita ya ufungaji bora Ligi Kuu bara inayodhaminiwa na benki ya NBC, inaweza kuwa mbichi kwani nyota wa timu kubwa na kongwe hapa nchini, Yanga na Simba hawapo kwenye kinyang' anyiro.
Lakini sasa mshambuliaji wa timu ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi, Francis Ngoy anaongoza kwa mabao mpaka sasa akiwa amepachika mabao 7.
Wanaomfuatia ni Saleh Karabaka ana mabao 6 na Paul Peter wote wa JKT Tanzania ana mabao 5, nyota wa Yanga ambaye ana mabao mengi zaidi ni Prince Dube ana mabao 4.
