Baada ya Tshabalala, Yanga kumng' oa Mpanzu Simba

Elie Mpanzu alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Simba SC mnamo Septemba 2024. Hadi sasa, amebakisha mwaka mmoja na chini ya miezi minane kukamilisha mkataba wake. Kwa mujibu wa taarifa, Mpanzu analipwa dola 7,000 kwa mwezi (takriban TSh milioni 18).

Hii inaifanya kuwa rahisi kwa klabu nyingine kumchukua kwa gharama ndogo — hasa kwa timu zenye uwezo mkubwa kifedha na zinazomfuatilia kwa karibu. Hapa ndipo hoja yangu ya mikataba mifupi kwa wachezaji bora inapojitokeza kwa nguvu.

Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kuwa huu ni udhaifu mkubwa katika upangaji wa muda mrefu wa vikosi vyetu. Mfano Bora: Azam FC Klabu ya Azam FC imekuwa mstari wa mbele katika kuweka misingi imara ya muda mrefu kwa kusaini mikataba mirefu na wachezaji wao.

Kwao, ni nadra sana kuona mchezaji akipewa miaka miwili.
Mara nyingi mikataba yao ni ya miaka mitatu au zaidi, jambo linalowapa utulivu na nafasi ya kupanga maendeleo ya timu bila presha ya kumpoteza mchezaji muhimu bure.

Simba SC, iwapo wanahitaji kuendelea kufurahia huduma ya Mpanzu, sasa ndio wakati sahihi wa kuanza maandalizi ya mkataba mpya. Msimu ujao unapoanza Agosti, utakapoisha mkataba wake utakuwa umebaki muda mfupi sana. Na kama hatakuwa amesaini mkataba mpya, anaweza kuondoka bure, jambo litakalokuwa pigo kwa klabu.

Note; (Mkataba wa Mpanzu unanunulika) Dube vs Yanga Feisal Vs Azam Hili sio kwa sababu Simba SC haina uwezo wa kifedha, bali ni kwa sababu uwezo alionao Mpanzu utawavuta wanunuzi wengi, wenye uwezo wa kutoa ofa kubwa zaidi ya ile Simba inamlipa sasa.